Inawezekana kabisa ya kuwa wewe unayesoma ujumbe huu hujaokoka - yaani
hujampokea Yesu Kristo ndani ya moyo wako kama Bwana na Mwokozi wako.
Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako.
Naamini
Roho Mtakatifu ameweka fursa hii mikononi mwako kwa mpango maalum wa
Mungu ili ufike mahali pa kutubu na kuokoka. Inawezekana kabisa, pia ya
kuwa hujawahi kuambiwa juu ya umuhimu wa wewe kuokoka. Lakini napenda
kukuambia ya kuwa ni mpango wa Mungu uokoke. Soma Wakolosai 1:13,14 na
Yohana 1:12-14 na 1 Timotheo 2:3-6 na Warumi 1:16,17 na Yohana 3:7. Ni
vigumu kuona baraka za Damu ya Yesu bila ya kuokoka.
Kwa
hiyo kama unataka kuokoka - tafuta mahali palipo na utulivu, na usome
kwa sauti sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala
hii)
“Ee
Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi.
Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha
yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika
msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi
yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo
nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na
Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na
kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za
maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la
Yesu Kristo. Amina.
Ikiwa
umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka
na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na
alivyoandika katika neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
Baada
ya kuokoka
Unapoanza
maisha haya mapya katika Yesu Kristo nakushauri mambo yafuatayo:
1.
Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7)
2.
Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11)
3.
Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi
8:14-17)
4.
Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7;
Zekaria 4:6)
5.
Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu
Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25)
6.
Soma jarida la "Hongera
kwa Kuokoka" linalopatikana kwa kubonyeza
HAPA.
Ukipenda unaweza
kuniandikia kwa anwani hii hapa chini juu ya uamuzi uliofikia leo wa
kuokoka, ili tumshukuru Mungu pamoja, na tuzidi kukuombea; na pia,
tukutumie maandiko mengine ya kukusaidia:
Christopher
Mwakasege,
S.L.P. 2166, ARUSHA, Tanzania.
Email: tasoet@nexusdigital.co.tz
S.L.P. 2166, ARUSHA, Tanzania.
Email: tasoet@nexusdigital.co.tz
No comments:
Post a Comment