UWEZA WA JINA LA YESU
Mtume
Paulo anasema katika Waraka wake kwa Wakolosai sura ya tatu na mstari wa
kumi na saba kuwa; “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo,
fanyeni yote katika JINA LA BWANA YESU, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.”
Hii ina maana ya kuwa, tukila tule katika Jina la Yesu Kristo. Tukilala
tulale katika Jina la Yesu Kristo. Tukizungumza tuzungumze katika jina
la Yesu Kristo. Tukiimba tuimbe katika jina la Yesu Kristo. Tukitembea
tutembee katika jina la Yesu Kristo. Tukisafiri tusafiri katika jina la
Yesu Kristo. Tukilima shambani tulime katika jina la Yesu Kristo; na
kadhalika.
Kwa nini tunatakiwa tufanye
mambo yote katika jina la Yesu Kristo? Jina hili la Yesu Kristo lina
sehemu gani katika maisha yetu ya kila siku?
Kama
tunatakiwa kufanya mambo yote katika jina la Yesu Kristo, kwa nini
hatufanyi hivyo?
Ukitafakari
maagizo tuliyopewa katika biblia utaona ya kuwa, maisha yetu yote
yanalitegemea jina hili la Yesu Kristo.
Kama
mambo yetu yote yanatakiwa yafanyike kwa jina la Yesu, basi ni muhimu
tujifunze zaidi na zaidi kila siku juu ya jina hili la ajabu.
Ni
maombi yangu kwa Mungu Baba, katika jina la Yesu Kristo ya kuwa maneno
yaliyomo katika somo hili yatachochea kwa upya kiu iliyomo ndani yako ya
kutaka kufahamu zaidi siri iliyomo ndani ya jina la Yesu Kristo.
Wiki ya Kwanza:
Jina
la Yesu Kristo - Mojawapo ya Funguo za Ufalme wa Mbinguni
Wiki ya Pili: Tafakari juu ya Jina la Yesu Kristo
Wiki ya Tatu: Yesu Kristo - Jina la Mwana wa Mungu
Wiki ya Nne: Mamlaka ya Jina la Yesu
Wiki ya Tano: Omba kwa Jina la Yesu Kristo
Wiki ya Sita: Umuhimu wa kuweka imani yako katika Jina la Yesu Kristo
Wiki ya Pili: Tafakari juu ya Jina la Yesu Kristo
Wiki ya Tatu: Yesu Kristo - Jina la Mwana wa Mungu
Wiki ya Nne: Mamlaka ya Jina la Yesu
Wiki ya Tano: Omba kwa Jina la Yesu Kristo
Wiki ya Sita: Umuhimu wa kuweka imani yako katika Jina la Yesu Kristo
No comments:
Post a Comment